You are on page 1of 1

HALMASHAURI YA MANISPAA TEMEKE

TANGAZO KWA UMMA JUU YA UUZAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA GOLANI KATA YA KIMBIJI NA YALEYALE PUNA KATA YA PEMBA MNAZI
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Kampuni ya Ardhi Plan inatangaza kuuza viwanja 1500 vilivyopimwa katika eneo la Golani Kata ya Kimbiji jirani na kambi ya JKT na Yale Yale Puna Kata ya Pemba Mnazi. Viwanja vyenye ukubwa na matumizi mbalimbali vitauzwa kwa mujibu wa bei zilizopo katika Jedwali la hapo chini kwa utaratibu ufuatao:i) ii) iii) iv) v) vi) vii) Fomu za maombi ya kumiliki kiwanja hazitalipiwa. Idadi ya fomu zilizoandaliwa inalingana na idadi ya viwanja vilivyopo. Fomu za maombi ya kumiliki viwanja zitatolewa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 9 Alasiri tarehe 02.04.2013 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Mwisho wa kurudisha fomu zilizojazwa kwa ukamilifu ni tarehe 08.04.2013 saa 9 Alasiri. Ankara za malipo (Vocha) pamoja na mwongozo wa kulipia viwanja zitatolewa kwa mwombaji atakayerudisha fomu kwa muda uliopangwa. Malipo yalipwe kwa mkupuo ndani ya siku 21. Mwombaji ambaye hatakuwa amefanya malipo kwa muda uliopangwa kiwanja husika kitatolewa kwa mwombaji mwingine bila ya taarifa yoyote kwake. Viwanja vilivyopangwa kwa ajili ya makazi vina ukubwa kama ifuatavyo: Na. 1 2 3 Aina Ujazo wa juu (High density) Ujazo wa Kati (Medium density) Ujazo wa Chini (Low density) Ukubwa (M2) 300-600 601-1200 1201-2500 Idadi 761 617 52 Gharama kwa kila Mita ya mraba 8,000/= 8,000/= 10,000/= 8,000/= 8,000/= 8,000/=

JEDWALI: VIWANGO VYA GHARAMA YA VIWANJA KWA MATUMIZI MBALIMBALI Na. Aina ya matumizi Idadi ya viwanja 1. Makazi pekee (Ujazo wa juu, kati na chini) 1222 2. Makazi na Biashara 206 3. 4. 5. 6. Biashara(Hotel, Vituo vya mafuta, maduka makubwa) Huduma za Jamii (Zahanati, shule ya awali,sekondari) Ibada/kuabudu Makazi maalumu(Housing Estate) 18 43 7 4

Imetolewa na: MKURUGENZI WA MANISPAA TEMEKE

You might also like