You are on page 1of 2

Ardhi mabingwa Safari Pool Dar. Na Mwandishi Wetu.

CHUO cha Ardhi jijini Dar es Salaam kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool ngazi ya mkoa katika mashindano ya yaliyoyoshirikisha Vyuo vya Elimu ya juu yajulikanayo kama Safari Pool Higher Learning Competition 2014 mwishoni mwa wiki katika Coco Beach. Ardhi ilifanikiwa kupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha CBE 1312, na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na nafasi ya kupeperusha bendera ya jiji la Dar es Salaam katika fainali za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mai 3 na 4,2014 mkoani Kilimanjaro. Nafasi ya pili ilichukuliwa na CBE ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/=,nafasi ya tatu ni Chuo UDSM ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/= na nafasi ya nne ni Chuo cha DUCE ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 100,000/= Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume, Steven Richard kutoka Chuo cha CBE alitwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/= pamoja na tiketi ya kuwalikisha mkoa wa Mwanza na mshindi wa pili ni Haji Hussein kutoka chuo cha IFM ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shiling 100,000/=.Upande wa wakinadada, Jacline Moleli kutoka Chuo cha TIA alifanikiwa kutwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 100,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha wakinadada mkoa kwenye fainali za kitaifa na nafasi ya pili ilichukuliwa na Salma Said kutoka Chuo cha CBE ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shililingi 50,000/=.

Fainali za Kitaifa zitashilikisha mikoa nane ambayo ni Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na wenyeji wa mashindano wa mwaka huu wa 2014,Mkoa wa Kilimanjaro.

You might also like