You are on page 1of 2

PRESS RELEASE

4/5/2016
First National Bank yafungua tawi Mwanza
Benki ya First National Bank Tanzania (FNB) imeendelea kupanua wigo kitaifa
kwa kufungua tawi jipya eneo la Rock City Mall jijini Mwanza leo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Francois
Botha alisema uzinduzi wa tawi la FNB Mwanza umelenga kukidhi ongezeko
kubwa la mahitaji ya huduma za kibenki na za kifedha katika mkoa huo.
Uzinduzi wa tawi la Mwanza ni sehemu ya uwekezaji endelevu na mkakati
wa kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha.
Pia tumezingatia ukuaji wa haraka wa mkoa wa Mwanzaambao una mchango
mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.
Botha alisema tawi Mwanza ni la tisa miongoni mwa mtandao wa matawi ya
FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mtandao wa
matawi ili kuyafikia maeneo yote nchini.
First National Bank daima tunafikiri njia mbalimbali za ambazo tunaweza
kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la Mwanza
litatoa ufumbuzi wa kina kwa wateja wanao ishi Mwanza na maeneo jirani
yenye biashara inayokua kwa kasi Botha alisema.
Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma
inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi
pamoja na biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu
wanaoishi jijini Mwanza na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi
zinazokua kwa kasi, alisema Botha.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella


alisema mkoa wa Mwanza una uwezo mkubwa wa kiuchumi na ukuaji
mkubwa wa sekta mbalimbali za kiuchumii karibuni ni ishara kuwa Mwanza
inakua kwa kasi.
"Tunakaribisha uwepo wa FNB na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha
huduma zenu hapa na mikoa mengine," alisema Mkuu wa Mkoa.
Alisema mbali na mkoa wa Mwanza kuwa na mchango mkubwa katika
maendeleo ya uchumi wa nchi bali pia inazalisha mali nyingi na ina utajiri
mkubwa wa rasilimali. Tunatarajia kuwa mtatoa mchango mkubwa katika
utoaji huduma za kifedha mkoani Mwanza kupitia huduma zenu mbalimbali
kwa kutumia ubunifu na utaalamu wenu, Mongella alisema.
Tawi hilo lililofunguliwa kwenye jingo jipya la Rock City Mall litatoa huduma
za kawaida za kibenki pamoja na huduma za dijitali kwa masaa 24 ili
mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara
katika eneo hilo.
MWISHO.
MAELEZO KWA WAHARIRI
First National Bank ni benki inayotoa huduma kwenye nchi mbalimbali barani
Afrika tangu mwaka 1874. Hivi sasa FNB inatoa huduma zake kwenye nchi za
Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Zambia, Mozambique, Lesotho, Swaziland
na Tanzania na mpango wake ni kuwa benki inayohudumia watu wengi zaidi
barani Afrika.
First National Bank Tanzania ilifungua milango yake rasmi nchini Tanzania
tarehe 27 Julai 2011, tawi la Mwanza likiwa ni la tisa, matawi mengine ni
pamoja na tawi la makao makuu, Mbezi Beach, Sinza, Mbagala, Quality
Centre, Peninsula, Kariakoo na tawi la Kimweri.
Kwa taarifa zaidi tembelea www.fnbtanzania.co.tz au tuma barua pepe
info@fnb.co.tz

You might also like